"Fahari ya Utu Wetu"

Breaking

Friday 30 December 2016

SIMULIZI: DEREVA TOYO sehemu ya 39

DEREVA TOYO
Sehemu Ya 39
Mtunzi...MoonBoy
Simu No.. +255714419487 Whatsapp
Ilipoishia Iliyopita..
"unamuambia nani we fala? au ushaanza kunizoea vibaya ee?"
"jemsii achana na huyo mke msaidie mama yako kwanza"
"mi naona ushaanza kunipanda kichwani we rey"
Sasa rey alinikazania nimseidie mama angu. Afu huku mke wangu na anasema
"we jemsi?"
"sema mke wangu nakuskia mamaa"
"mimi na mama yako nani unampenda zaidi"
"aaahhh jamani si wewe mamiii"
"basi naomba tuingie ndani"
"Eeh ehh unasema?"
"Eeh Eeh nini? Nimesema tuingie ndani haraka"
ENDELEA→→↓
Kiukweli nilikua fala zaidi ya fala maana mke wangu alinishauri ujinga mtupu..na kwa jinsi nilivyo fala nikakubali kuingia ndani na kumuacha mama yangu pale nje akiwa ametulia chini... sijui kafa
"we jemsi?"
"sema mke wangu nakuskia mamaa"
"mimi na mama yako nani unampenda zaidi"
"aaahhh jamani si wewe mamiii"
"basi naomba tuingie ndani"
"Eeh ehh unasema?"
"Eeh Eeh nini? Nimesema tuingie ndani haraka"
"sawa mke wangu nimekuskia twende zetu"
Huezi amini nilimuacha mama angu pale nje akiwa kalala chini. Tuliingia ndani na kuendelea na furaha yetu huku tukiwa na mziki mkubwaa kwa kupata kiasi kikubwa cha fedha, Mke wangu kwa furaha alionayo aliniahidi leo atanipa ndoa leo usiku, Basi mke wangu alipika HUBWA HUBWA NA MAHARAGWE NA NYAMA tukiwa tunakula hapo mezani huku mziki mkubwa ukilindima katika geto letu. Mke wangu alianza kunipangia kazi za kufanya kwa siku ya kesho. ili kesho kutwa asafiri kumpelekea mama yake pesa,
"kesho ukimaliza kuosha vyombo hakikisha unaenda kuchukua maziwa unayachemsha afu bila kukosa supu kwa pembeni... ili nikiamka nivipate mume wangu au sio?"
"sawa mke wangu ila si tuchukue lita moja na mimi ninywe?"
"ah ah we kunywa chai ya kawaida tu"
"mmhh sawa mke wangu kwani nakuskiliza wewe tu"
"naaaa kesho mida ya saa 4 ufue nguo zote ili keshokutwa nisafiri nikiwa msafi"
"sawa lakini si niende kwanza kazini ili nirudi mchana kuzifua?"
"basi usicheleww sawa?"
"sawa mke wangu"
Unajua swala la kuosha vyombo humu ndani. hua nalifanyaga kila siku toka nilipoanza kutikisika ubongo, mpaka leo yapata kama mwwzi hivi naa.... hajawahi kugusa vyombo zaidi ya leo asubuhi. na ni kwasababu ya ile dozi ya jana usiku na ndio mana sikuosha vyombo. ila naoshaga, Sasa tulipomaliza kula mke wangu alipanda kitandani kisha akawa anachati wasapu... Maana sasa hivi si anaitumia ile SAMSUNG GALAXY S4 YANGU hivyo na yeye siku hizi yupo bize na kuchati, Sasa akiwa anaendelea kuchati mara alipigiwa simu na mtu nisiemjua wala kumsikia... Aliipokea simu na kuanza kuongea nae.... ila huyo mtu simjui kwahio haya ni maongezi tu ya mke wangu
"halloo mpenzi mambo?"
"?????"
"mi mzima tu"
"?????"
"shida gani tena mpenzi?"
"??????"
"aaaaaahh Ni hilo tu?"
"?????"
"basi ngoja nitakutumia laki 4 keshokutwa sawa?"
"??????"
"ok bai bai bayby"
"?????"
"nawe pia"
Alipomaliza nilianza kumuuliza maswali mengi tu
"huyo uliokua unaongea nae ni nani?"
"ni rafiki yangu wa kike hua tuna tabia ya kuitana mpenzi"
"aaaaa hahahahaha kumbe? na huyo baby je?"
"aaa huyo nimemuita baby kwasababu yeye kamaliza miaka mitatu, maana si unajua mjini kila mtu baby?"
"aaahhhh kumbe ndio ule mseemooooo"
"ndio huo"
"kwaio ana shida na pesa?"
"ndio mume wangu si alinikopesha laki 4 nikasuke nywele sasa... ndio ksniambia nimrudishie"
"okeee.... sasa na mimi si uniite baby maana nami nipo mjini"
"noo kwani wewe una miaka mingapi hapa mjini?"
"mmhhh sikumbukia ila ni kama miaka 15 hivi"
"basi hadi ufikishe 20 ndio uitwe baby"
"haaaa je nikifa?"
"ukifa si tutakuita hayati"
"Eeeehhh na hilo pia ni jina la kimahaba?"
"ndio...ila ni hadi ufe"
"sasa nitaftie basi na mimi jina la kuniita wewe"
"labda nikuite fala"
"Eeee? jina gani ilo mke wangu? si matusi ayo?"
"sikiliza mume wangu.... wale wanaosema fala ni matusi ujue hawajasoma wakamaliza elimu yao vizuri"
"mmhhh lakini mke wangu fala ni tusi aiseee"
"jamani mumewangu fala sio tusi, fala ni neno la ndani ya ndoa ila halipaswi kutaamkwa hovyo hovyo na ndio maana watu wanaliona kama ni tusi"
"Oookeeee kuumbeee? Kwaio fala tafsiri yake ni nini?"
"yaani fala linamaanisha neno I LOVE YOU"
"haaaaa kweli?"
"ndio... kwaio kama nikikuita we fala ujue nimekwambia (I LOVE YOU)"
"duuu yaanu mke wangu ndio kwanza unanifumbua macho"
"afu pia kama nikikuita we fala na wewe unasema (ILOVE YOU TOO) maana neno fala linasema ilove you"
"kwaio ukiniita fala nami niseme ilove you too? kwasababu umeniita na neno ilove you?"
"ndio mume wangu.. kua mjanjaa"
Basi hayo yalikua ni maongezi baina yangu na mke wangu... Kiukweli maisha nilikua nayaona matamu sana kua na mke kama huyu...
BAADA YA SIKU HIO KUPITA
Na leo ni siku nyingine tena mida ya saa 4 asubuhi nikiwa zangu kijiweni nakula vichwa tu... tena leo ilikua ni mwisho wa mwezi, hivyo nilikua nazungukia baadhi ya pesa zangu ambazo hua nalipwagwa kwa mwezi, nilifanya zoezi hilo huku nikifurahi kweli maana mke wangu alikua akinipenda sana... Na licha ya hivyo pia maisha yalikua ni matamu na maraisi mno. Hivyo nami nilikua nampenda sana mke wangu... Japo mwanzo nilikua namuona kama lijitu linene. lakini kwa sasa kawa miss tanzania, yaani anavutia ile mbaya,
Basi ilipofika mida ya mchana nilikumbuka kua nina nguo za kufua kule nyumbani, hivyo nilielekea kwa baba toyo na kuiacha toyo kisha nikampa pesa nusu,
"we vp mbona leo unanipa elfu 10?"
"mbona huulizi kwanini nimerudi saa hii?"
"kwahio una maana gani kijana?"
"nina maana ya kwamba? nimefanya kazi nusu siku"
"kwahio na pesa nayo unanipa nusu?"
"ndio?"
"mi naona umechoka kazi we kijana"
"we mzee? ivi huna hata huruma wewe Eeh?"
"huruma gani?"
"wenzangu woote madereva toyo wanawalipa mabosi zao shilingi Elfu 7 kwa siku nzima...leo nakupa Elfu 10 kwa nusu siku... afu unaanza mdomo? basi sitaki tena toyo yako... afu tuone kama kuna mtu ataweza kukupa elfu 20 kwa siku"
"ah ah kijana lakini hatugombani bwana... usiache kazi kijana"
"kwanza mjomba wangu keshanunua toyo siku nyingi tu sema ni wewe tu ndio unanizuga zuga wewe"
"basi kijana usiache kazi"
"naacha"
"basi nipe elfu 15 kwa siku"
"nitakufikiria"
Basi nilikua nampa mzee jamba jamba. maana anazidi kunikontroo akili yangu, ..... Sasa moja kwa moja nilielekea nyumbani huku nikiwa nina kiasi cha laki mbili na nusu, ambacho nimelipwa na wateja watatu. wanaonilipa kwa mwezi, Ila sio maingizo ya leo Kwani leo nimeingiza Elfu 20 tu kwa abiria kadhaa. na hata hivyo ni kwamba nimefanya kazi nusu. ili niwahai nyumbani....
Basi nilifika nyumbani na kukusanya nguo zote chafu kisha nikazitoa hapo nje. na kuanza kuzifua kwa umakini kweli, Nikisachi suruali za mke wangu nakutana na kondom za kike.... ila sikufatilia sana maana huenda alizinunua kwa ajili yetu sisi...
Yaani nilikua nina nguo nyingi hizo, Maana mke wangu ana kama wiki mbili hajafua kabisa.
Sasa nikiwa naendelea kufua fua, mara rey akatokea na kunisalimia
"jemsi mambo?"
"poa tu"
"hizi nguo ni unafua mwenyewe au upo na mke wako?"
"kwani we unatakaje?"
"we si unijibu tu?"
"nipo mwwnyewe"
"mungu wangu jemsi wangu si utaumia jamani?"
"umeanza unoko rey Ee?"
"mmmhh basi tuachane nayo...vp mkeo yupo?"
"hayupo kwani vp?"
"jemsi? ivi unajua hali ya mama ako?"
"kwani ana nini?"
"si vile alivyodondoka jana pale"
"heeeeee sasa si kadondoka mwenyewe? kwani mi inaniusu nini?"
"jemsi utapata laana wewe, yaani jana mama ako anaseidiwa na majirani afu nyie mnatekenyana tu huko ndani?"
"sasa unakoelekea rey nitakuziba mibao sasa hivi"
"sawa tu. ila mama yako yupo ndani kesharudi hospitali"
Sasa rey aliondoka baada ya kuniona nimeanza kubadirika kwa hssira. lakini alipoelekea naona anaenda kule kwa mama angu. Nilishindwa kuelewa ni kwanini aende kule.... Basi rey aliingia mpaka ndani kwa wazazi wangu kisha sikujua kilichoendele. ila pazia lilivyofunuliwa na ubaridi nilimuona rey akiwa kapiga magoti mbele ya mama angu... huku kama vile anaomba msamaha kwa kosa fulani alilolifanya... sikuelewa kinachoendelea pale ndani. Sasa wakiwa wanaombana kama msamaha... Mara mke wangu karudi Basi nilimkimbilia na kumpokea kipima joto chake (kibegi cha kwapani Nilikiingiza ndani kisha nikatoka nje...
"za kazi mke wangu?"
"aaahh safi tu"
Aliingia ndani huku akiwa amenuna nuna ila kwakua najua furaha yake.. nilijisemea kua
"ngoja nimalize kufua nije nikupe mkwanja maana najua ndicho kilichokununisha"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kufua nguo za mke wangu... Mara aliniita kwa jina lile lenye tafsiri ya Ilove you...
"we fala?"
"i love you toi mke wangu unasemaje?"
"umechukua na zile chupi zangu?"
"ndio mke wangu mpaka zile taiti pia nafua hapa"
"ok zifue vizuri afu uje uzianikie huku ndani sawa?"
"lakini mke wangu? si una chupi nyingine?"
"ndio ninazo kwani vp?"
"aaaa nilijua unataka kuvaa kauka nkuvae"
"mschiuuuu we fala kweli wewe"
"i love you too mke wangu"
Alikua kila akisema fala nami natakiwa niseme ilove you too...kwasababu fala lina maana ya ilove you
Basi nilifua nguo mpaka nimechoka ile mbaya kwani nguo zilikua ni nyingi mno, Sasa baada ya muda nilimuona rey akitoka kule kwa mama na kuzunguka nyuma nyuma kisha sikumuona tena,
Baada ya muda nilimuona mama angu akitoka nje huku akiangalia huku nilipo mimi.... Mara akamuita mke wangu
"mama saidi?"
Lakini kwakua sauti ilikua haifiki mpaka huku geto hivyo mimi nilifanya kama kumuita mke wangu ili nimuambie unaitwa
"mke wangu?"
"nini na wewe?"
"mama anakuita kule"
"ananiitia nini tena?"
"sijui"
Mke wangu akatoka nje huku akijipodoa podoa...
"limama lako nalo lina tabu duuu"
"au kama vp usiende"
"acha nikalisikilize tu"
"kua makini mke wangu, maana usikute keshakua mchawi huyo"
Daaahh Eti mama angu namuita mchawi aisee duu, Kweli hii ni shida
Sasa baada ya kama dakika kama tano rey alikuja hadi pale nilipo na kuanza kusema utumbo tumbo wake
"we jemsi?"
"nini? afu umerudi tena eeh?"
"mke wako kaenda kufanya nini kule?"
"sijui bhanaa"
"sasa mi nataka nikuambie ukweli juu yako"
"ukweli wa nini?"
"kuusu mke wako"
"kafanya nini? niambie kafanya nini?"
Sasa rey yeye alikua akitoa sauti ya chini lakini mimi nikawa natumia sauti ya kufoka foka kwa sauti mpaka mke wangu akasikia
"tulia sasa usipige kelele jemsi"
"nisipige kelele nini? Mke wangu Eeeee? njoo umuone mnafiki wako huyu hapa"
Sasa mke wangu kuskia hivyo alikurupuka kule bila hata kuaga.. kisha akaja pale na kuniuliza
"unasemaje we fala?"
"i love you too mke wangu...ni huyu rey eti anasema aniambie kitu kuusu wewe"
"kitu gani hicho?"
"muulize mwenyewe"
Sasa mke wangu akamgeukia rey na kuanza kuongea kwa kusutana
"Rey? unataka kunivunjia ndoa yangu ee?"
"wewe batuli hebu kua na huruma hata kidogo basi.... yaani minguo yote hii ya wiki mbili nzima anafua peke yake?"
"ndio kwani inakuusu? tayari keshakua fala huyu"
"Eeee I love you too mke wangu...muambie huyo anajua wapi maana ya fala huyo...afu we rey unatuzoea ee?"
"heee yaani mpaka unamuita fala?"
"sikiliza rey...mambo yetu mimi na wewe yalishakwishaga hivyo naomba usinijue jue tena"
"Eee mwambie uyo asitujue jue"
Nilikua naingilia ingilia maongezi yao pale
"ila batuli wenzio hawafanyi hivyo wewe?"
"sasa kwani yanakuusu jamani rey?'
"najua hayaniusu lakini nami nilikubali kwasababu nilijua kutakua na faida juu yangu lakini naona unanitolea matusi tu"
"lakini si nilikulipa pesa yako?"
"sawaaa lakini mimi sikufanya kwaajili ya pesa"
Sasa nikawa siyaelewi maongezi yao maana naona kama wanaongea biashara fulani hivi......
"kwahio we rey unatakaje?"
"muachie mtoto wa watu"
Mmhhh sasa nikaingilia kati kwa mambo nisio yajua
"kwani kamchukua mtoto wa nani?"
"we nawe hayakuusu...endelea kufua"
"kwahio batuli utamuachia mtoto wa watu au utapunguza?"
"kumuachia simuachii na pia kupunguza sipunguzi... kwani unataka nini?"
Heee mara mke wangu akaanza kufunga nguo vizuri ili wapigane pale pale nje... na muda huo ilikua ni mida ya saa 9 hivi alasili. Sasa kabla hawajaanza kupigana Nilimuona mama angu akimnyooshea rey mkono kua akimbie... Ila tukio hilo mke wangu hakuliona. Hivyo rey alikimbia kama vile kamuogopa mke wangu.... lakini mi najua kaambiwa na mama angu akimbie. Sasa baada ya rey kukimbia Wacha mke wangu acheke huku akijisifu
"Heeheee huuwezi mziki wangu... mbona umekimbia? njoo kama wewe ni mwanamke kweli, unajishauwaa njoo sasa nikuonyeshe watu wanapigwaje"
"ndio mke wangu ungemzibua kabisa maana kazidi unoko"
"na wewe fala hebu fua uko"
"i love you too mke wangu, namalizia hizi chache tu"
"fanya haraka nipo ndani"
Sasa alipokua anaingia ndani mara kaitwa tena na mama angu
"jamani mama saidi hatujamaliza kuongea"
"Aaahhh kumbe? ni hili li rey ndio limenichefua akili"
Hivyo mke wangu akagairisha kuingia ndani na kuenda kule kwa mama angu.... Kisha wakaingia ndani huku wakizungumza kitu.. ila sikusikia kwa kua palikua pana hatua kadhaa kidogo......
Sasa nikiwa naendelea kufua pale nje mara Rey kapita mbio na kuingia chumbani kwetu.... Sasa nikajiuliza huyu rey mbona kaingia huku geto tena kwa spidi kweli... Niliacha kufua kisha nikaelekea kule ndani kwetu.... yaani kwenye chumba nilicho pangisha....
Sasa nikawa nanyata ili nimuone anaiba nini....
Mara katoka huku akiwa kama kuna kitu kashika kwa nyuma....
"we umechukua nini huku ndani?"
Nilimuuliza huku nikiwa namsogelea ili niangalie alichoiba na kukiweka nyuma nyuma....
"rey si nakuuliza umechukua nini huko ndani?"
Sasa rey kule alipogeuzia mgongo ndio mke wangu alipo hivyo kama mke wangu ataangalia huku, basi atakiona alichokishika rey kwa nyuma....... Nilichokifanya ni kumuita mke wangu ili aone hicho kitu kilichoshikwa na rey......
"mama saidiiiiii?"
Sasa nilipomuita tu... nikaona kafunua pazia... Heee saa ngapi hajakiona hicho kilichoshikwa na rey....
Nilimuona mke wangu akija spidi hio ili amshike rey... na kumpokonya kile alichokishika rey... huku mke wangu akimsihi rey kua
"reiiiiiiiii pliiiizi usifanye hivyo"
Alikua akiongea huku akija kwa spidi ya hatari...
"rey nakuomba dada angu usifanye hivyo"
Sasa mke wangu alipokua anamkaribia rey kwa kumkamata Aaaiiisee mke wangu alichelewa kumfikia rey.....hivyo rey aliniambia niangalie nyuma kuna mtu ananinyemelea.... Lakini nilipoangalia nyuma hakukua na mtu wala nini.... Sasa ile nageuka tu ili nimuulize huyo mtu yupo wapi.... Aiseeee rey Alini............
Lakini baada ya kitendo hicho alichokifanya rey... nilimuoa mke wangu kakosa nguvu ghafla na kuduwaa kama dudu zeeee vile
Je? unajua Rey kashika nini?
Na je? Alinifanya nini?
Na ni kwanini mke wangu kakosa nguvu ghafla?
USIKOSE SEHEMU YA MWISHO YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA
SEHEMU YA 40
KARIBUNI KUENDELEA KUIFUATILIA
SIMULIZI MPYA YA NIPE YOTE
INAYOENDELEA KURUSHWA KWENYE BLOG YAKO PENDWA...AHSANTENI.

No comments:

Post a Comment